Dk. Nchimbi kuzindua jengo jipya JNIA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, atazindua rasmi jengo la wageni mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, Januari 16, 2026.
Jengo hilo, lililojengwa kwa fedha za Serikali katika Terminal 1, limekamilika kwa asilimia 100 na litalenga kuhudumia viongozi wa kitaifa, wakuu wa nchi za kigeni na wageni mashuhuri. Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaji Abubakar Kunenge, amewahimiza wananchi kushiriki uzinduzi huo utakaohudhuriwa na viongozi mbalimbali.
RC Kunenge amesema ujenzi wa jengo hili umetoa ajira kwa vijana wengi na litachangia ukuaji wa uchumi wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla, huku likiongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji na utalii. SOMA: Mwanza na mikakati ya uwanja wa ndege wa Kimataifa



