Dk. Samia aahidi kujenga soko la samaki la kimataifa Tanga

TANGA: Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa endapo atapewa tena dhamana ya kuongoza nchi, Serikali yake itaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa soko la samaki la kimataifa katika eneo la Pangani, mkoani Tanga, wenye gharama ya shilingi bilioni 1.3.

Akizungumza leo Septemba 29, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Pangani, Dk. Samia ameeleza kuwa soko hilo litajengwa katika Kata ya Kipumbwi, na litakuwa chachu ya maendeleo kwa kuongeza kipato cha wavuvi na wafanyabiashara, hivyo kukuza uchumi wa wilaya hiyo.

Aidha, Dk. Samia ameahidi pia kukamilisha ujenzi wa barabara inayounganisha Wilaya ya Bagamoyo hadi Tanga, hususan vipande vya Pangani–Saadani na Makurunge.

Vilevile, ameweka msisitizo katika kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi ili ziwe za kisasa zaidi na ziweze kufikia viwango vya kimataifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button