Dk. Samia: Kila mtanzania atapa maji safi na salama

TANGA: MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kuimarisha sekta ya maji nchini kwa lengo la kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yake.

Ahadi hiyo ameitoa leo, Septemba 29, 2025, wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya Gombero, wilayani Pangani, mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Dk. Samia amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake, sekta ya maji imepiga hatua kubwa, na kusisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita itaendeleza jitihada hizo kwa kuhakikisha miradi ya maji inawafikia wananchi wa mijini na vijijini moja kwa moja.

Katika hotuba hiyo, Dk. Samia pia ametumia fursa hiyo kumpongeza mgombea ubunge wa jimbo la Pangani kwa juhudi zake madhubuti katika kuendeleza miradi ya maji wilayani humo. Amesema kuwa mgombea huyo ni kijana makini, mwenye dhamira ya kweli na aliyethibitisha uwezo wake katika kusimamia miradi inayowanufaisha wananchi.

Aidha, Dk. Samia ametumia muda mfupi kuwaomba wananchi wa Pangani kumpigia kura mgombea huyo ili aweze kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan sekta ya maji. Aliahidi kuwa iwapo atachaguliwa tena, serikali yake itaendelea kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yake, kwa lengo la kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button