Dk Tulia awasili Marekani ziara ya kikazi

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson

NEW YORK: Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson, amewasili New York nchini Marekani leo Februari 8, 2024 kwa ziara ya kikazi.

Dk Tulia Ackson amepokelewa na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa nchini Marekani Dk Suleiman Haji Suleiman.

Akiwa nchini humo, Dk Tulia anatarajia kuongoza mkutano wa Kibunge wa Umoja wa Mabunge Duniani katika Umoja wa Mataifa pamoja na kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi Wakuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Advertisement

Mkutano huo wa kibunge unahudhuriwa na Maspika na Wakuu wa misafara ya Mabunge 180 duniani na unatarajiwa kuangazia jukumu maalum la kibunge kwa kushirikiana na Mamlaka za Kiserikali katika kuchagiza mijadala ya kuleta amani duniani.