Dkt Ashatu Kijaji ziarani Ghana

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mazingira, Teknolojia na Ubunifu wa Ghana Ophelia Hayford. Dkt. Kijaji yupo nchini Ghana kwa ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu katika biashara ya Kaboni.