BASI lililobeba wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Dodoma Jiji limepinduka na kutumbukia mtoni katika eneo la Nangurukuru mkoani Lindi likiwa na wachezaji.
Ajali hiyo imetokea leo Februari 10, 2025 ambapo kikosi hicho kilikuwa kikitokea Ruangwa mkoani Lindi kurejea mkoani Dodoma, baada ya mchezo wao wa jana wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Fortunatus Johnson amethibitisha tukio hilo akieleza kuwa wachezaji wote wamejeruhiwa kwa kukatwa na vioo vya gari.
Taarifa zinaeleza kuwa mpaka sasa hakuna kifo kilichoripotiwa, na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu.