Dodoma waombea amani kuelekea uchaguzi Mkuu

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewahadharisha wanaofikiria kuharibu amani ya mkoa huo kuelekea. Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka huu. Senyamule alieleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa mkoa huo katika mkutano maalumu wa kuliombea amani taifa kuelekea uchaguzi mkuu.

“Kazi yetu tuliyo nayo sasa sisi kama mabalozi wa amani au ambao tuna uchungu na tunatamani kuona amani ya Mkoa wa Dodoma, ni hakika kila mmoja aende akamwambie mwenzake kuwa sisi tumekiri kuwa Mkoa wa Dodoma tunataka amani hatutakuwa tayari kuona mtu anaharibu amani hapa,” alisema na kuongeza: “Na kama wapo waliokuwa wanadhani na kufikiria kuwa sisi tuharibu amani ya Dodoma tunawaambia kuwa sisi wana Dodoma tunataka amani, kama unataka kuharibu amani toka nje ya mipaka ya Dodoma kapoteze amani mahali pengine,” alisema. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali, makundi ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama.

Ulitanguliwa pia na matembezi maalumu ya amani yaliyoanzia katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma na kuishia kwenye Viwanja vya Nyerere yakiwa na kaulimbiu ya mkoa, ‘Umejiandikisha kapige kura, Nimejiandikisha nitapiga kura. SOMA: Watu 435,119 kupiga kura Arusha Mjini

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button