Watu 435,119 kupiga kura Arusha Mjini

ARUSHA: Watu 435,119 wanatarajia kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, kwenye vituo vya kupiga kura 1,051 Jimbo la Arusha Mjini.

Aidha, kwa mpiga kura aliyepoteza kadi yake na ambaye aliandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura ataruhusiwa kupiga kura kwenye kituo alichopangiwa akiwa na leseni ya udereva, hati ya kusafiria au kutambilisho cha NIDA.

Lakini pia majina ya kitambulisho mbadala atakachowasilisha ambacho majina yanapaswa kufanana na yaliyomo katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Akizungumza na wanahabari jana jijini Arusha, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini, Shaban Manyama amesema vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura ndivyo vitakavyotumika kupiga kura ambavyo vitafunguliwa saa 1 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button