Tume yakutana na mwakilishi UN

TUME ya Uchunguzi ya matukio ya uvunjifu wa amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imekutana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Parfait Onanga Anyanga.
Parfait Onanga amewasili nchini kwa ziara ya kikazi inayolenga kufanya mashauriano na Serikali pamoja na wadau mbalimbali kuhusu hali ya kisiasa nchini kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025. SOMA: Tume ya uchunguzi yakutana na Abdurahman Kinana

Tume hiyo inaendelea na mahojiano na waathirika wa matukio hayo baada ya hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi kuiongezea muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026, ili Tume iweze kukamilisha kazi yake. Tume inatakiwa kukamilisha na kuwasilisha ripoti yake kabla au ifikapo tarehe 3 Aprili, 2026.




