Wanasiasa wanaimani Tume ya Jaji Chande
BAADHI ya wanasiasa wameeleza imani yao kuwa majibu sahihi kuhusu chanzo cha vurugu zilizotokea Oktoba 29 mwaka jana yatapatikana kupitia Tume Huru ya Uchunguzi iliyoundwa na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan.
Wameshauri kuwa taarifa itakayotolewa na tume hiyo, iliyoundwa Novemba 8 mwaka jana chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Mkuu mstaafu Mohammed Chande Othman, inapaswa kupokewa na kuheshimiwa na Watanzania. Akizungumza na gazeti la Uhuru , Mbunge wa Manyoni, John Chiligati, alisema Rais Dk. Samia alifanya jambo la busara na kistaarabu kwa kuunda tume hiyo kuchunguza vurugu hizo.
Amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya kutafuta ukweli na suluhisho la kudumu kwa changamoto hiyo. “Tukio hilo lililotokea ndani ya nchi linapaswa kushughulikiwa na kutatuliwa ndani ya nchi yenyewe,” alisema. Ameongeza kuwa Watanzania wana uwezo wa kujadiliana na kupata majibu bila kuhitaji uamuzi kutoka nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Chiligati, tume halisi ni wananchi wenyewe, hivyo aliwataka Watanzania kuwa watulivu wakisubiri matokeo ya uchunguzi huo yatakayopendekeza namna ya kuepuka matatizo kama hayo kujirudia. Amesema vurugu zina madhara kwa ustawi wa taifa na kushauri changamoto zinapotokea zitafutiwe suluhisho la amani badala ya kutumia nguvu.
Amebainisha kuwa vurugu husababisha hasara kubwa kiuchumi na kuharibu uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi na washirika wake, hivyo mazungumzo na maridhiano ndiyo njia bora ya kujenga mshikamano na kulinda maslahi ya taifa.
Akizungumzia matukio ya vurugu za Oktoba 29 kabla na baada ya uchaguzi, alisema hayapaswi kuathiri maendeleo na mshikamano, huku akitoa wito kwa wananchi na viongozi kushirikiana kulinda amani na utulivu. Amesema siasa ni mfumo unaogusa kila nyanja ya jamii na kutoa mwelekeo wa maisha ya wananchi na ustawi wa taifa kwa ujumla.

Amefafanua kuwa mazingira ya kisiasa huathiri moja kwa moja namna watu wanavyoishi na kufanya maamuzi ya kila siku, huku akisisitiza kuwa siasa bora hujenga mazingira rafiki ya kiuchumi, kijamii na kiutawala. SOMA: Serikali yaja mpango wa kitaifa wa maridhiano
Naye Balozi mstaafu na Meja Jenerali mstaafu, Gaudence Milanzi, amesema tume hiyo inapaswa kuachwa ifanye kazi kwa uhuru wake. Amesema wananchi wanapaswa kuiamini tume hiyo na kuwa na subira, kwani kazi yake inahitaji utulivu na muda wa kutosha ili kufikia hitimisho lenye tija kwa taifa.
Amesisitiza kuwa siasa haipaswi kuwa maneno matupu, bali chombo cha kuboresha maisha ya watu kwa vitendo vinavyoonekana. Aidha, ameeleza umuhimu wa kuhakikisha huduma muhimu za miundombinu, afya na elimu zinapatikana kwa usawa kwa wananchi wa vijijini na mijini. Ameongeza kuwa siasa si suala la kumridhisha kila mtu, bali kufanya maamuzi sahihi, hata kama ni magumu, kwa ajili ya maendeleo ya kudumu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, amesema wananchi wanapaswa kupokea taarifa ya tume kwa utulivu na umakini. Amesema matokeo ya tume hiyo yanapaswa kuwa fursa ya kujifunza na kujitathmini kama taifa. Ameeleza kuwa anaamini tume hiyo itatoa ukweli utakaosaidia kuimarisha mshikamano wa jamii.
Ameongeza kuwa matokeo hayo yanaweza kuwa chachu ya kutatua matatizo ya muda mrefu kulingana na mapendekezo yatakayowasilishwa. Amewataka wananchi na viongozi kutumia matokeo hayo kama mwongozo wa kujenga mustakabali bora wenye amani, uwajibikaji na maendeleo endelevu.
Amesema mazingira ya kisiasa yanapokuwa tulivu na shirikishi, hutoa fursa kwa kila mtu kushiriki bila hofu, jambo linaloimarisha demokrasia na kuongeza uwajibikaji wa viongozi. Amebainisha kuwa vurugu za Oktoba 29 zimeharibu taswira ya siasa kwa kiasi kikubwa na kusababisha baadhi ya wananchi kudhani siasa ni uadui.

Amesisitiza umuhimu wa kurejesha heshima ya siasa kwa kujenga utamaduni wa majadiliano ya amani na kuheshimiana. Naye mwanasiasa mkongwe, Hamad Rashid, amesema ana matarajio makubwa na tume hiyo kutokana na kuwajumuisha watu makini na wazalendo. “Ni wazi kabisa tume itatoa majibu yatakayosaidia na kueleza umuhimu wa kulinda taifa letu,” alisema.
Wajumbe wa tume hiyo ni pamoja na Jaji Mkuu mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, IGP mstaafu Said Mwema, Dk. Stergomena Tax, Paul Meela na Luteni Jenerali mstaafu. Novemba 20 mwaka jana, Rais Dk. Samia aliizindua tume hiyo ili kuchunguza matukio hayo. Hata hivyo, Februari 21 mwaka huu, tume iliongezewa muda wa siku 42, huku ripoti yake ikitarajiwa kuwasilishwa mwezi ujao.

Machi 11 mwaka huu, Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Parfait Onanga-Anyanga, aliwasilisha salamu za Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres, Ikulu Chamwino, Dodoma. Amesema Umoja wa Mataifa unatambua na kupongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania kufuatia matukio ya Oktoba 29, ikiwemo kuundwa kwa tume hiyo na kuendelezwa kwa mazungumzo ya kitaifa.
Aidha, alieleza kuwa Umoja huo unaendelea kuitambua Tanzania kama nchi yenye historia ya amani, utulivu wa kisiasa na mshikamano wa kitaifa. Kwa upande wake, Rais Dk. Samia amesema serikali imejizatiti kuhakikisha mchakato wa uchunguzi unafanyika kwa kuzingatia misingi ya utawala wa sheria, uwajibikaji na haki.
Amesema serikali iko tayari kupokea na kufanyia kazi mapendekezo yatakayowasilishwa na tume hiyo, ikiwa ni pamoja na yale yatakayosaidia kuimarisha maridhiano ya kitaifa na mabadiliko ya kikatiba. Amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa pamoja na jumuiya za kimataifa katika kukuza demokrasia, utawala bora na maendeleo jumuishi.



JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com