Serikali yaja mpango wa kitaifa wa maridhiano

SERIKALI ya Tanzania imeeleza nia ya kuanzisha Mpango wa Kitaifa wa Maridhiano ili kuponya mipasuko ya kijamii na kuimarisha majadiliano miongoni mwa wananchi. Pendekezo hilo liliwasilishwa na Beatrice Mpembo, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kutoa Taarifa ya Haki za Binadamu katika Wizara ya Katiba na Sheria, wakati wa kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Mpembo alisema mpango huo unalenga kuhimiza ukweli na majadiliano, kushughulikia malalamiko ya kihistoria, kuzuia migogoro ya baadaye na kuimarisha utawala wa kidemokrasia na umoja wa taifa. SOMA: Tume yakutana na mwakilishi UN

Hii inafuatia hatua za Serikali zilizochukuliwa kufuatia vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, ikiwemo kuundwa kwa Tume Huru ya Uchunguzi wa Vurugu za Uchaguzi iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Tume hiyo, inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, inachunguza chanzo cha vurugu, uharibifu wa mali, madai ya vifo na kupendekeza hatua stahiki za kurekebisha na kuimarisha uwajibikaji wa taasisi za umma. Mpembo amesema tume imezingatia pia hatua za vyombo vya usalama na mapendekezo ya mageuzi ya kuzuia matukio kama hayo katika uchaguzi ujao.

Aidha, vijana 1,787 waliobainika kufanya makosa madogo walipewa msamaha, na wizara ya vijana chini ya Ofisi ya Rais imeanzishwa kushughulikia changamoto zao za ajira, maendeleo ya ujuzi na uwezeshaji. Mpembo amesema tume ilipewa siku 90 kukamilisha kazi yake, lakini muda uliguzwa kwa siku 42 kutokana na mwitikio wa wananchi. Taarifa ya mwisho ya tume inatarajiwa kuwasilishwa Aprili, 2026.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button