Wanaojihusisha mapenzi ya jinsia moja watengwe’

KIGOMA: Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, MaryPrisca Mahundi ameitaka jamii kuwatenga watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ubakaji na ulawiti.

Naibu Waziri Mahundi amesema hayo wakati wa kongamano la wadau wa kupinga ukatili mkoani Kigoma akijibu tuhuma na malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wadau wa kupinga ukatili wakiitaka serikali kuchukua hatua kwani mambo hayo yanayoonekana kama yanafumbiwa macho na serikali na ndiyo maana vitendo hivyo vinaendelea.

Akijibu tuhuma na malalamiko hayo, Naibu Waziri Mahundi amesema kuwa serikali imeweka sheria kali na hatua zimekuwa zikichukuliwa kila taarifa inapotolewa kuwepo kwa vitendo hivyo na kubainisha kwamba jamii ndiyo yenyewe jukumu la kutoa taarifa kuhusu uwepo wa watu wanaofanya vitendo hivyo.

Akizungumza katika kongamano hilo, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, Mussa Maulid ameitaka serikali kusimamia kwa karibu makosa ya ushoga ili watu wanaohusika na masuala hayo wapewe adhabu kali ili kuinusuru jamii na vitendo vya mmomonyoko wa maadili vinavyotokana na ushoga, ulawiti na ubakaji.

Meya huyo wa Manispaa ya Kigoma Ujiji alisema kuwa binafsi aliamua kulivalia njuga vitendo vya ushoga na kuwafuata baadhi ya watu wanaotuhumiwa kwa vitendo hivyo lakini alishangazwa na majibu ya watu hao kumtaka asiwafuatilie kwani miili wanayotumia kufanya hivyo ni ya kwao na wamepewa na Mungu.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Baraza Kuu la Waislamu mkoa Kigoma, Shekhe Harun Shaharawi amesema mmomonyoko wa maadili wa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ubakaji na ulawiti vimeufanya mji wa Ujiji ambao ulikuwa ukisifika kwa ustaarabu na maadili ya kiafrika kwa sasa umechafuka ikiwemo kufanyika kwa sherehe za kitaifa za mashoga mambo ambayo yanaharibu maadili na mila za mji huo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. FLY88 là nền tảng giải trí trực tuyến hàng đầu, mang đến cho người dùng kho trò chơi đa dạng cùng tỷ lệ thưởng cực kỳ hấp dẫn. Hệ thống được thiết kế với giao diện mượt mà, tối ưu hóa trải nghiệm trên mọi thiết bị di động và đảm bảo tính minh bạch tuyệt đối.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button