DR CONGO: WATU wasiopungua 12 wameuawa katika mashambulizi mapya ya waasi wa kundi la ADF lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mashambulizi hayo yanatokea baada ya mfululizo wa mashambulizi mengine ya ADF katika kipindi cha Krismasi ambao watu 21 waliuawakatika jimbo la Kivu Kaskazini.
Maafisa wa eneo hilo wamesema mashambulizi hayo yametokea usiku wa kuamkia Jumatano na yalilenga maeneo mawili katika jimbo moja.
Afisa mmoja Samuel Kagheni, amelieleza shirika la habari la AFP kwamba waasi hao waliwaua watu wanane katika kijiji cha Bilendu.
Watu wengine wanne waliuawa katika kijiji cha Mangoya, huku waasi wakiendelea kuchoma nyumba katika maeneo yote mawili.SOMA: Rwanda Congo wakubaliana kumaliza mivutano