Shambulio la mazishi laua watu 50

KIVU KASKAZINI, DRC : ZAIDI ya watu 50 wameuawa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya kushambuliwa kwa mapanga na waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF), linaloungwa mkono na kundi linalojiita Dola la Kiislamu (Islamic State), wakati wa mazishi katika kijiji cha Ntoyo, wilayani Lubero.

Afisa wa serikali katika eneo hilo, Macaire Sivikunula, alisema shambulio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana. SOMA: Mauaji mapya ya ADF yatikisa DRC

Kwa upande wake, msimamizi wa kijeshi wa Lubero, Kanali Alain Kiwewa, aliwaambia waandishi wa habari kwamba idadi ya vifo imefikia takribani watu 60 na huenda ikaongezeka kwani baadhi ya wakazi bado hawajulikani walipo. ADF ni miongoni mwa makundi yenye silaha yanayopigania ardhi na rasilimali katika eneo la mashariki mwa DRC, ambalo lina utajiri mkubwa wa madini.

Jeshi la serikali ya DRC likishirikiana na majeshi ya Uganda, limesema limeimarisha operesheni za kijeshi dhidi ya kundi hilo katika wiki za karibuni. Tukio hili linakuja mwezi mmoja tu baada ya ADF kuwaua watu zaidi ya 50, na pia kuhusishwa na shambulio jingine lililosababisha vifo vya watu 38 katika kanisa mnamo mwezi Julai.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.

    This is my main concern………………. http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button