Droo kufuzu Afcon Morocco 2025 kupangwa Julai 4

AFRIKA KUSINI – DROO ya kufuzu kwa michuano ya fainali ya Mataifa ya Afrika, Morocco mwaka 2025 itafanyika Julai 4, Johannesburg, Afrika Kusini.

Mataifa 48 wakiwemo washindi wanne wa hatua ya awali Chad, Eswatini, Liberia na Sudan Kusini watapangwa kwenye makundi 12 kuwania nafasi ya kushiriki fainali hizo.

Mataifa yaliyothibitishwa kwa droo hiyo ni pamoja na mabingwa watetezi Ivory Coast, Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Comoro, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Misri, Guinea ya Ikweta, Eswatini na Ethiopia.

Mataifa mengine ni Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea Bissau, Kenya, Lesotho, Liberia, Libya, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Morocco, Msumbiji, Namibia, Niger, Nigeria, Rwanda, Sao Tome & Principe, Senegal, Sierra Leone, Afrika Kusini, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Togo, Tunisia, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Mechi za kufuzu zinatarajiwa kuanza Septemba mwaka huu kupata mataifa 24 yatakayoshiriki fainali hizo zitakazofanyika Morocco mwaka 2025

Habari Zifananazo

Back to top button