Dugange: Fuatilieni afya zenu kama AFCON

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Dk Festo Dugange

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dk Festo Dugange amewakumbusha wananume kufuatilia afya zao na Afya za Watoto kama wanavyofuatilia michuano ya Mataifa ya Africa AFCON2023 inayoendelea nchini Ivory Coast.

Michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Januari 13, Tanzania ilishuka dimbani jana na kunyukwa bao 3-0 na Morocco.

Dk Dugange ameitoa kauli hiyo katika uwanja wa Mbagala Zakhem mkoani Dar Es Salaam wakati akizundua zoezi la uchunguzi wa Afya na Chanjo kwa wananchi,

Advertisement

“Tunamwamko mkubwa katika kufuatilia michezo hususani AFCON2023 tunapenda sasa mwamko huo akinababa wenzangu kujali na kulinda afya kinga kwa Watoto maana akinamama wametuzidi mbali juu ya Afya ya Watoto wetu na kuzingatia Afya zao wenyewe,”amesema.

Zoezi hilo linaloendelea katika viwanja hivyo limeratibiwa na Shirika la Johs Hopkins University (JHU) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION unaofadhiliwa na USAID kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Afya