DAR-ES-SALAAM: Shindano la wazi la Mchezo wa Gofu”KCB East Africa Golf Tour” Linatarajiwa kufanyika Agosti 3 katika Klabu ya Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania-JWTZ Lugalo Gofu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Leo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ Lugalo Gofu amesema, shindano nila siku moja linatarajia kupata wawakirishi watakoecheza finali.
“Shindano ni la siku moja huku likiwa na lengo la kupata Wachezaji wanne watakaoiwakilisha nchi kwenye Fainali za Michuano hiyo nchini Kenya.”amesema Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo (Mwenyekiti Lugalo Gofu)
Kwa Upande wake Meja Japhet Masai Nahodha wa Lugalo Gofu amesema, Shindano Hilo litachezwa Kwa Mfumo wa Kimataifa wa “Stable Ford” ambapo Mshindi atapatikana Kwa kuhesabu Alama kwenye Kila shimo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa KCB Bank Tanzania Cosmos Kimario amesema, shindano Hilo litakuwa likifanyika Kila Mwaka huku lengo likiwa ni kuendeleza Michezo nchini hasa Mchezo wa Gofu.
SOMA: Lugalo Golf Fundraiser’ kusisimua gofu kwa watoto
Shindano la “KCB East Africa Tour” Linatarajiwa kufanyika Agosti 3,2024 likiwa na lengo la kutafuta Wachezaji wanne watakao iwakikisha nchi kwenye Fainali nchini Kenya.
SOMA: https://www.bbc.com/swahili/michezo/2015/04/150427_tanzania_golftournament