MTAYARISHAJI na muongozaji wa filamu ya kisayansi ya Eonii, Eddie Mzale amewataka watayarishaji wa filamu nchini kuacha woga wa kuandaa filamu bora kwa kisingizio cha kutoweza kumudu gharama za kamera kubwa na zenye ubora.
Eddie Mzale amesena waandaaji wengi wa filamu nchini ukiwauliza kwa nini hawandai filamu za kisayansi watasema hawana vifaa vya kufanya hivyo zikiwemo kamera.
“Waache uongo, woga na hofu ni kweli ukiwa na kamera yenye ubora mkubwa na filamu yako inakuwa nzuri lakini filamu si camera tu kuna vitu vingi vikifanyika pamoja ndiyo unapata filamu bora si kamera tupu” anasema Eddie.
Eddie Mzale anaongeza kwamba katika filamu yake ya Eonii inayoshikilia tuzo ya filamu bora ukanda wa Afrika Mashariki katika tuzo za filamu za ZIFF 2023 anasema yeye ametumia kamera ndogo na ya kawaida katika kuandaa filamu hiyo ili awatie moyo waongozaji wengine wa filamu nao wafanye filamu za kisayansi na waache kutoa sababu zisizo na msingi wa kujenga sana ya filamu nchini.
“Watu wengi wananiuliza kamera nilizotumia katika filamu yangu ya kisayansi ya Eonii wanadhani nimetumia kamera aina ya red kumbe nimetumia kamera ya kawaida tu lakini nimejua namna ya kuitumia ili nipate filamu bora yenye picha bora nikafanikiwa watayarishaji wengine waige na watambue kwamba katika filamu kamera ni sehemu tu ya kuelekea ukamilishaji wa filamu ila vitu vingi vinachangia kupata ubora wa picha ya filamu na si kamera tupu,” anasisitiza Eddie.
Comments are closed.