Elimu usalama barabarani kwa wanafunzi Shinyanga

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Ushirika, iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga, wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuepuka ajali wanapoenda au wanaporudi shuleni.
Akitoa elimu hiyo kwa wanafunzi, askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, Sajenti Aneth Mutafuta, amewaasa kuacha tabia ya kucheza au kufanya michezo katika maeneo ya barabara.
Pia amewafundisha jinsi ya kuvuka barabara kwa usalama kupitia vivuko vya watembea kwa miguu.