Ewura yataka Mamlaka za Maji kutoa taarifa sahihi

Mkurugenzi Mkuu wa  EWURA Mhandisi Modestus Lumato, amezitaka Mamlaka za Maji nchini kuhakikisha zinatoa taarifa sahihi za huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wananchi ili kushamirisha upatikanaji wa huduma endelevu ya maji.

Lumato ametoa maelekezo hayo leo Nov.14,  2022, jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa  25 na Miradi ya Kitaifa 7 kilicholenga  kuhakiki taarifa za utendaji wa mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22.

Tathmini iliyofanywa na EWURA imebaini kuwapo mamlaka za maji ambazo zimeendelea kuwasilisha taarifa zenye mapungufu kwenye kukidhi viwango vya huduma, uchakavu, ufanisi wa makusanyo ya maduhuli na muda wa upatikanaji wa huduma.

 

Habari Zifananazo

Back to top button