FCC kuongeza uelewa haki, wajibu

DAR ES SALAAM: TUME ya Ushindani (FCC) imetangaza kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki ya Mlaji Duniani kwa kuendesha kampeni maalumu ya utoaji elimu kwa walaji na wafanyabiashara ili kuongeza uelewa wa haki na wajibu wao katika soko.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Khadija Ngasongwa amesema maadhimisho hayo yanalenga kuwawezesha walaji kufanya maamuzi sahihi wanaponunua bidhaa au huduma, pamoja na kuwahamasisha kuchukua hatua pale wanapobaini ukiukwaji wa sheria.

Amesema elimu hiyo pia itawalenga wafanyabiashara kwa kuwajengea uelewa kuhusu wajibu wao wa kumlinda mlaji na kuzingatia matakwa ya sheria katika utoaji wa bidhaa na huduma.

Kwa mujibu wa FCC, kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Machi 31, 2026 katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga.

Amesema katika maadhimisho ya mwaka huu, tume hiyo imejikita kutoa elimu kupitia vipindi vya redio na televisheni, pamoja na majukwaa ya mitandao ya kijamii ili kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, FCC itaendesha kliniki za walaji katika mikoa ya Pwani, Dodoma, Musoma, Njombe na Tanga kwa lengo la kupokea na kushughulikia hoja, malalamiko na changamoto zinazowakabili walaji.

Sambamba na hilo, Machi 10, 2026 Tume hiyo itaendesha semina kwa wafanyabiashara na taasisi zinazotumia mikataba ya walaji (Standard Form Consumer Contracts) katika ofisi zake za Dar es Salaam, ili kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa mikataba inayozingatia haki za mlaji.

Vilevile, Machi 11, 2026 kutafanyika semina kwa wadau wa sekta ya ujenzi wakiwemo wazalishaji wa nondo, bati, nyaya za umeme na rangi za majumbani, pamoja na vyama vya kibiashara na wadhibiti wa kisekta.

Mbali na semina hizo, FCC itatumia magari ya matangazo (road shows) kufikisha elimu kwa wananchi moja kwa moja katika maeneo yao.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo amewahimiza wananchi wenye changamoto zozote zinazohusiana na bidhaa au huduma kufuatilia vipindi vya elimu vitakavyorushwa na vyombo vya habari, kuhudhuria kliniki za walaji na kutumia fursa hiyo kuwasilisha malalamiko yao kwa ajili ya kupatiwa ufafanuzi au hatua stahiki.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  https://www.payathome9.place

  3. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button