Fella ammwagia sifa Sir Nature

MENEJA wa msanii, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ amemmwagia sifa rapa mkongwe, Juma Kassim ‘Sir Nature’ akidai ni mwanamuziki mzuri na bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kubamba.

Fella ambaye awali alikuwa meneja wa msanii huyo kabla ya kuhitilafiana takribani miaka 15 iliyopita, ameeleza kuwa ni mambo machache anahitaji kuyaweka sawa ili kuendelea kuonesha ubora wake.

Alisema hata wakati wanaingia kwenye mgogoro alifahamu wanachoshindania kuhusu maslahi hakikuwa na uhalisia kama kinavyoelezwa japokuwa alifahamu Nature ni msanii mkali mno.

“Yaliyotokea mengine Mungu kayapanga, mengine tumesababisha sisi wenyewe, maana yake wakati ule watu walikuwa wanazungumzia maslahi, lakini ukiangalia wakati ule muziki maslahi hakuna na ilifika wakati huwezi ukazungumza kwamba hakuna maslahi.

“Lakini ukimzungumzia Nature ni msanii mzuri sana, sana na Inshaallah atafanya vizuri, kuna vichache tu na uzuri nilishamwita hapa nyumbani, nimemshauri nikamwambia akiwa na lolote aje nimshauri,” alisema Fella ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilungule, Mbagala.

Habari Zifananazo

Back to top button