FIFA, Uefa zilikosea kuzuia Super League

MAHAKAMA barani Ulaya imeamua kwamba UEFA na FIFA zilikuwa kinyume na sheria kwa kuzuia uundaji wa mashindano ya Super League mnamo 2021.

Klabu za Real Madrid na Barcelona zimethibitisha kwa mara nyingine tena uungaji mkono wao kamili kwenye Super League.

Mkurugenzi Mtendaji wa Super League, Bernd Reicart amesema klabu sasa zinaweza kuamua ushiriki wao kwenye michuano hiyo.

“Uefa ukiritimba umekwisha. Kandanda ni bure. Vilabu sasa viko huru kutokana na tishio la kuwekewa vikwazo na viko huru kuamua mustakabali wao katika Super League”.amesema Reicart.

Man United, Atlético, PSG, Bayern pamoja na vilabu vya La Liga vikiwemo Sevilla, Valencia, Villarreal vimetangaza kutounga mkono michuano hiyo.

La Liga na Ligue1 zote zilitoa taarifa ya kutounga mkono Super League sambamba na Serikali ya Uingereza.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button