G7 kujadili nishati ya umeme Ukraine

ULAYA : MAWAZIRI wa nishati wa kundi la nchi saba zilizoinukia zaidi kiviwanda (G7) watakutana siku ya Jumatatu ili kujadili hali ya miundombinu ya nishati ya umeme ya Ukraine iliyoharibiwa vibaya na vita.

Tangu uvamizi kamili wa Moscow mnamo Februari 2022, mifumo ya nishati ya Ukraine imekuwa ikilengwa na mashambulizi ya Urusi na kusababisha matatizo ya ugavi wa umeme.

Umoja wa Ulaya umesema unalenga kuikopesha Ukraine kiasi cha dola bilioni 39 kutoka kwa mapato ya mali za Urusi yaliyozuiwa katika umoja huo.

Advertisement

Norway, kwa upande wake, imesema itaongeza msaada wa kiraia kwa Ukraine dola milioni 475 na kutanua mpango wake wa msaada kwa miaka mitatu hadi 2030.

SOMA : EU wakubaliana kusaidia $54bn Ukraine