Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mrisho Gambo amemkaribisha nchini aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema ili kuchuana kwenye siasa “karibu tufanye siasa za kistaarabu.” Ameandika Gambo.
Gambo ameandika ujumbe huo leo, Machi 1, 2023 kupitia ukurasa wake wa Twitter akiweka picha aliyopiga pamoja na Lema na kuandika na kuongeza “Karibu nyumbani Mhe Godbless Lema. Siasa za ushindani zina raha yake.” Ameandika Gambo.
Lema aliwahi kuwa mbunge wa Arusha Mjini kipindi Gambo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2020, Gambo alishinda uchaguzi huo dhidi ya Lema wa Chadema ambaye baada ya uchaguzi huo Lema alidai kutishiwa maisha na kuamua kutimkia Nairobi Kenya na baadaye kwenda Canada.