Gara B atuma salamu Basata

DAR ES SALAAM; MSHEREHESHAJI wa matukio mbalimbali nchini Godfrey Deogratius Rugalabamu maarufu ‘Gara B’, ameliomba Baraza la Sanaa (BASATA) kuandaa mpango wa kufahamika rasmi washereheshaji ili pia watumike katika matukio ya kitaifa.

Akizungumza na HabariLEO mapema leo, Gara B ambaye pia ni mwigizaji amesema ikibidi serikali iandae tuzo ambazo zitawatambua.

“Unajua tuko wengi sana Tanzania nzima na tunahudumia jamii kwa namna kubwa zaidi,” amesema Gara B.

Gara B ameishukuru Serikali kwa kuweka mifumo mbalimbali katika maeneo mengi yanayowezesha urahisi wa utendaji kazi wao.

Mtangzaji huyo wa kipindi cha ‘Mr Right Show’ amesema licha ya vipaji vyote alivyonavyo ila ameegemea zaidi kwenye ushereheshaji kutokana na wingi wa mahitaji.

Habari Zifananazo

Back to top button