Warembo 15 kuwania Miss Kinondoni 2026

DAR ES SALAAM: Warembo 15 wanataraajia kuwania taji la Miss Kinondoni 2026, katika fainali inayotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia maandalizi ya mashindano hayo, Mkurugenzi wa Kampuni ya SPM Entertainment , Salome Kikwembe, amesema maandalizi yanaendelea vizuri huku wakijipanga kuhakikisha mashindano ya mwaka huu yanakuwa na ushindani mkubwa.

Kikwembe amesema moja ya malengo yao ni kuandaa mshiriki atakayekuwa na uwezo wa kufanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania na hatimaye kutwaa taji hilo la taifa.

“Tumeshanza maandalizi ambapo warembo wapo kambini kujinoa kwa mashindano. Fainali ya mwaka huu itakuwa ya aina yake. Tunajivunia warembo wenye sifa ambao wana uwezo wa kupambana na kutwaa taji la Miss Tanzania,” amesema Kikwembe..

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button