Gavana BoT afurahishwa ushirikiano ZEEA mikopo bila riba

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba amependa ushirikiano unaofanywa baina ya Kampuni Airpay Tanzania na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) katika kuwafanya wananchi kurejesha mikopo ya bila riba inayotolewa na Serikali ya Zanzibar.

Ushirika huo wa ZEEA na Airpay ambayo ni Kampuni yenye lengo la kurahisisha mifumo ya malipo ya kifedha kidijitali kwa watu wa kawaida Wafanyabiasha na wajasiliamali wadogo wadogo inaelezwa kuwa utasaidia wakopaji kurejesha na kukopa fedha kwa wakati.

Gavana Tutuba ameyasema hayo juziJijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha BoT, ZEEA, Airpay pamoja na wadau mbalimbali kutoka Taasisi za kibenki na mitandao ya simu.

Advertisement

Alisema amefurahi kuona ZEEA wanashirikiana na Airpay katika kuleta mfumo wa kidijitali ili kusaidia namna nzuri ya kuwafanya wakopaji kurejesha fedha zinazotolewa na serikali bila riba ili ziweze kusaidia wananchi wengine na kwamba imani yake mfumo huo utasaidia urejeshwaji wa pesa kwa wakati.

Naye Mihayo Wilmore kiongozi upande wa Mifumo kutoka Airpay Tanzania alisema kitu wanachotaka kukifanya ni kuhakikisha mteja hapati usumbufu katika urejeshaji.

Juma Burhan Mohamed Mkurugenzi Mtendaji ZEEA alisema, wao kama wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi washatoa mikopo yenye thamani ya sh Bilioni 34.9 ambao umewafikia wanawake 14,000 na wanaume 9,000.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *