Gawio Mashirika, Taasisi za Umma laongezeka 68%

KUFIKIA Juni 09, 2025 Gawio la Mashirika na Taasisi za Umma kwenda Mfuko Mkuu wa Serikali limeongezeka kutoka sh bilioni 601 mwaka jana hadi sh trilioni 1.28 mwaka huu ambalo ni sawa na asilimia 68.

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu Dar es Slaam leo Juni 10 wakati akiwasilisha ripoti ya Gawio la Taasisi na Mashirika ya Umma kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam.

“Gawio hili ni la kihistoria. Haikuwahi kutokea Ofisi ya Hazina kukusanya kiasi kama hiki kufikia Sh trilioni 1,” amesema Mchechu na kuongeza kuwa jumla ya Mashirika na Taasisi za Serikali ni 309.

Amesema, gawio hilo linatarajiwa kuongezeka kwa kuwa ni taasisi na mashirikia 213 pekee yaliyowasilisha gawio kati ya 309.

Amesema, mafanikio yanayopatikana ni utekelezaji wa maagizo na maono ya Rais Samia ya mageuzi kwenye Mashirika na Taasisi za Umma katika hafla kama hii mwaka jana Juni 11.

Wakati huo huo Mchechu amesema mapato ya Benki ya NBC yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 600 kutoka sh bilioni 1.3 hadi sh bilioni 10.5 ikiwa ni matokeo ya maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaka mageuzi kwenye uendeshaji wa Mashirika na Taasisi za Umma.

Mchechu amesema, makampuni mengine yaliyofanya vizuri ni Benki ya CRDB kwa kuongeza mapato kutoka sh bilioni 16 mwaka jana hadi sh bilioni 64.

PUMA imeongeza mapato kutoka sh bilioni 8 hadi sh bilioni 12.

Gawio la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) limeongezeka kutoka sh bilioni 153 hadi sh bilioni 181.

Katika hatua nyingine Mchechu amesema Shirika la Twiga Mineral limeibuka kinara wa Mashirika sita ya Kibiashara yaliyotoa gawio kubwa zaidi serikalini kwa kuchangia jumla ya sh bilioni 93.6 kati ya sh trilioni 1.28 ya gawio lote la Mashirika na Taasisi za Umma kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwenda Mfuko Mkuu wa Serikali.

Akitaja mashirika hayo yaliyokabidhiwa tuzo na Rais Samia Suluhu Hassan, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema gawio la mwaka huu limepiku lile la mwaka jana la sh bilioni 601.

Nafasi ya pili ni Airtel Tanzania na Airtel Money waliotoa gawio la sh bilioni 73.9.

Benki ya NMB imetoa gawio la sh bilioni 68.1 hivyo kuwa namba tatu ya orodha hiyo ikifuatiwa na PUMA Energy waliochangia Sh bilioni 13.5.

TPDC imechangia sh bilioni 11.7 na NBC imechangia sh bilioni 10.5 ikiwa ni mashirika ambayo mwaka jana hayakuwepo kwenye ramani.

Mchechu amesema, kati ya Mashirika na Taasisi 309 zilizo chini ya serikali.

Mashirika 253 serikali inamiliki hisa nyingi ‘majority shares’ wakati mashirika 56 serikali inamiliki hisa chache ‘minority shares’.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button