Geay atakiwa kuibeba Tanzania riadha Berlin

UJERUMANI: BALOZI wa Tanzania, nchini Ujerumani, Hassan Mwamweta amemtaka mwanariadha, Gabriel Geay na wenzake kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya BMW Berlin-Marathon 2025 kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo, yatakayofanyika Septemba 21, 2025Berlin, Ujerumani.

Balozi Mwamweta alitoa kauli hiyo alipokutana na wanariadha hao, wakiongozwa na Gabriel Geay ofisini kwake jijini Berlin Septemba 19, 2025.

Balozi Mwamweta amesema mashindano ya BMW Berlin-Marathon ni miongoni mwa mashindano makubwa ya riadha Duniani ambayo mwaka huu yatajumuisha washiriki 80,000 kutoka duniani kote, hivyo, ushindi wa aina yotote utailetea heshima na kuitangaza nchi ya Tanzania ulimwenguni.

Balozi Mwamweta amewatakia heri wakimbiaji hao katika mashindano hayo na kuwaahidi kuwapa ushirikiano unaohitajika ili waweze kuwakilisha vyema bendera ya taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button