Geita Gold na juhudi za uwezeshaji wanawake

Geita Gold Mining Limited (GGML) imeendelea kuonyesha jitihada zake za kuwezesha wanawake katika maeneo mbalimbali ya maisha, kwa kutumia kila fursa ya kuinua wanawake katika ya shughuli zake na jamii kwa ujumla.

Kampuni hiyo imekuwa ikitoa kipaumbele kwenye mipango inayochangia maendeleo ya wanawake, na kutanabaisha uwezo wa mwanamke katika sekta ambayo kihistoria imekuwa ikiongozwa na wanaume.

Kihistoria, sekta ya madini duniani kote imekuwa ikitawaliwa na wanaume kwa mfano, nchi yenye migodi mingi zaidi ina uwakilishi wa wanawake wa asilimia 16 kwenye migodi yake, kwa Tanzania GGML imepiga hatua kubwa kwa kuhamasisha ushiriki wa wanawake kupitia mipango mbalimbali.

Kama kampuni tanzu ya AngloGold Ashanti, ambayo inaonyesha dhamira ya kufikia usawa wa kijinsia, imekuwa na wanawake kadhaa kwenye ngazi za juu za uongozi ambapo kurugenzi za fedha, sheria na rasilimali watu zinaongozwa na wanawake.

Kwa upande wa mgodi wa dhahabu wa Geita wanawake wanaunda asilimia 13 ya wafanyikazi wa GGML, jambo linaloonyesha juhudi kubwa za kampuni hiyo katika kuleta usawa wa kijinsia.

Ili kufanikisha malengo yake ya kukuza usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake katika nafasi za uongozi, GGML pia ilikuwa mdau muhimu katika kufanikisha maadhimisho ya miaka 10 ya Female Future Program na Mkutano wa 7 wa ATE wa uongozi (7th Annual Leadership Conference) ya mwaka 2025, iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) hali inayoashiria hatua muhimu katika kufanikisha usawa wa kijinsia mahali pa kazi.

Katika kipindi cha miaka minane ya ushirikiano wa GGML na ATE, Mpango wa Female Future umeongeza uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za usimamizi kutoka asilimia 0 hadi asilimia tisa.

Miongoni mwa wahitimu wa Female Future Program ni Janeth Luponelo, ambaye amekuwa akitajwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Meneja Mkuu wa Jiolojia na Utafiti katika kampuni GGML.

Kufanikiwa kwake kushika nafasi ya uongozi ni mfano wa ufanisi wa mpango huo katika kusaidia wanawake kuvunja vikwazo na kufanikisha malengo yao ya kazi.

Simon Shayo, Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti,anayesimamia uendelevu anasisitiza umuhimu wa mpango huu kwa kusema, “Tunajivunia kufadhili hafla hii muhimu, ambayo inalingana na malengo yetu ya kuwezesha wanawake na wasichana nchini Tanzania.

Mpango wa Female Future umekuwa muhimu katika kuvunja vikwazo na kutengeneza fursa za wanawake kufanikiwa katika uongozi. Kupitia mipango kama hii, tunaendelea kushirikiana katika kukuza usawa na ujumuishaji mahali pa kazi na zaidi.”

Duran Archery, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, anasisitiza mafanikio ya mpango huo: “Kwa kuwapa wanawake ujuzi muhimu wa uongozi, na ujuzi wa usimamizi wa juu, Mpango wa Female Future sio tu unagusa ukuaji wa mtu binafsi bali pia unabadilisha mahali pa kazi na kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia unakuwa jambo muhimu katika mfumo wa biashara badala ya kuwa la matumaini tu.” anaeleza na kusisitiza kwamba kukuza usawa wa kijinsia kunasababisha uboreshaji wa utendaji wa kampuni.

Mpango wa Female Future unatumika kama msingi wa dhamira ya GGML ya kukuza usawa, na ujumuishaji, ikiwa imefanya kazi pamoja na ATE kwa miaka minane. Katika kipindi hiki, mpango huo umeongeza uwakilishi wa wanawake katika nafasi za usimamizi wa juu kutoka asilimia 0 hadi asilimia tisa.

Mafanikio hayo yanaonyesha juhudi za mpango na ahadi ya mashirika yanayoshiriki katika kuendeleza uwakilishi wa wanawake katika ulimwengu wa biashara.Mkakati wa GGML kwa usawa wa kijinsia unagusa uwanda mpana hadi kwenye mpango wake wa mafunzo, ambapo inalenga usawa wa kijinsia kati ya wanaoomba nafasi mbali mbali, ikiwa waombaji wana sifa sawa, wanawake watapewa kipaumbele.

Mpango wa Female Future, pamoja na mipango inayoongozwa na ATE, imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuwezesha wanawake kufika katika nafasi za usimamizi na uongozi ndani ya GGML.

Zaidi ya hayo, kampuni hiyo imezindua kampeni mbili kuu: moja inayolenga kukomesha tabia zisizofaa na nyingine inayolenga kuongeza ufahamu wa kukomesha unyanyasaji wa kijinsia mahali pa kazi.

Wafanyakazi wanaopatikana na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia hufukuzwa kazi mara moja, jambo linaloonyesha sera kali ya GGML ya kutokubali unyanyasaji wa kijinsia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button