Gereza la Guantanamo kupokea wahamiaji Elfu Thelathini

MAREKANI : RAIS  wa Marekani, Donald Trump, ametangaza mipango ya kuandaa kituo cha kuzuilia wakimbizi katika gereza la kijeshi la Guantanamo, kwa ajili ya wakimbizi 30,000.

Kituo hicho, ambacho ni tofauti na gereza lenye ulinzi mkali, kimetumika hapo awali kuhifadhi wakimbizi, wakiwemo Wahaiti na Wacuba waliokamatwa baharini.

Hatua hii inakuja kwa lengo la kudhibiti  uhamiaji haramu nchini Marekani . SOMA: Trump afungiwa kusitisha ufadhili wa serikali

Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, ameielezea mipango hiyo kuwa ya ukatili, akidai kuwa wakimbizi hao watawekwa karibu na vituo vilivyotumika kwa mateso na vifungo vinavyokiuka sheria.

Wakati huo huo, vyama vya wafanyakazi  vya serikali nchini humo vimewashauri wanachama wake kuwa makini na pendekezo la Trump la kujiuzulu kwa hiari ambapo Rais  Donald  Trump  ametoa ofa ya kuwalipa mshahara wa miezi minane na marupurupu kwa lengo la kupunguza idadi ya wafanyakazi serikalini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button