Gofu Lina Tour yasaidia kuboresha viwanja

DAR ES SALAAM; MASHINDANO ya gofu ya Lina PG Tour yanayofanyika katika viwanja vya gofu vya klabu ya Moshi Gymkhana, yamesaidia kufufua mchezo huo na kuboresha viwanja hivyo baada ya kutokuwepo kwa miaka mingi.

Chimbuko la mashindani hayo ni kumuenzi muasisi wa maendeleo ya gofu ya wanawake nchini, Lina Nkya, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya gofu aliyefariki dunia miaka minne iliyopita.

Akizungumza mjini Moshi leo Mkurugenzi wa mashindano hayo ya Lina PG Tour, Yasmin Chali amesema kuwepo kwa michuano hiyo kumesaidia kufufua mchezo huo ambao umekuwa haufanyika mara kwa mara mjini hapo.

“Kuwepo kwa Lina PG Tour kumefufua viwanja kwasababu vilikuwepo lakini michezo haifanyiki na vilikauka, mashindano yamesababisha viwanja kuboreshwa na kufanyika ambapo yameweza kuvuta hata wachezaji kutoka Kenya,” amesema Challi.

Isome pia: ‘Lugalo Golf Fundraiser’ kusisimua gofu kwa watoto

Kwa mujibu wa Chali, viwanja vya gofu vya Moshi Gymkhana vilikuwa vimetelekezwa kwani hakukuwa na mashindano yoyote makubwa kwa miaka mingi.

Tayari mashindano hayo yameshafanyika sehemu tofauti ambapo ilianzia katika viwanja vya TPC Februari mwaka huu, Viwanja vya gofu vya Morogoro Gymkhana na Arusha.

Habari Zifananazo

Back to top button