GOMA: Waasi wa M23 wateka uwanja wa ndege wa Goma

GOMA: KUNDI la waasi wa M23 limeutwaa uwanja wa ndege wa Goma, ambapo sasa unashikiliwa na waasi hao, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari.
“Wamechukua udhibiti wa uwanja wa ndege, wapiganaji wa M23 wapo,” AFP imenukuu.
Zaidi ya wanajeshi 1,200 wa Congo wamejisalimisha na sasa wanashikiliwa katika kambi ya Umoja wa Mataifa iliyoko katika uwanja wa ndege.
Hatahivyo vyanzo vingine vya usalama na kidiplomasia vimeripoti kuhusu M23 kushikilia uwanja wa ndege wa Goma.



