Guinea waanza kuomboleza siku tatu

GUINEA : RAIA wa Guinea wameanza  kuomboleza kitaifa kwa siku tatu kufuatia vifo vya takriban watu 56 katika mkanyagano uliotokea uwanjani kwenye mji wa N’Zerekore Kusini-mashariki.

Waziri Mkuu Amadou Oury Bah amesema bendera za taifa zitapeperushwa nusu mlingoti  wakati wote wa maombolezo. SOMA: Mashabiki wa soka 56 wapoteza maisha

Mvutano ulizuka wakati wa mechi ya kandanda Jumapili wiki hii kufuatia uamuzi wa kutatanisha wa mwamuzi.

Advertisement

Baadhi ya mashabiki walioshuhudia wamesema  mashabiki walio na ghadhabu walirusha mawe, na kusababisha hofu na msongamano na mkanyagano katika uwanja huo.

Mashindano ya kandanda yaliandaliwa kwa heshima ya kiongozi wa kijeshi Jenerali Mamady Doumbouya, lakini upinzani ulikashifu serikali ya kijeshi kwa kutumia michezo kisiasa.

Walidai kuwa mashindano hayo yalikuwa ni mbinu ya kupendelea uwezekano wa Jenerali Doumbouya kugombea wakati wa uchaguzi ambao haujatangazwa.

Katika taarifa yake Rais alitangaza kuwa uchunguzi utaanzishwa ili kubaini chanzo cha mkasa huo huku akiwataka wananchi kuwa watulivu.