Haaland afikisha mabao 100

BAO la Erling Haaland alilofunga jana limekuwa bao lake la 100 akiwa na Manchester City katika mchezo ulioisha sare ya 2-2 dhidi ya Arsenal, uwanja wa Etihad.

Mshambuliaji huyo wa Norway alicheza mechi yake ya 105 katika kipindi cha miaka miwili.

Advertisement

Haaland alifunga bao hilo dakika ya tisa, akipokea pasi kutoka kwa Sávio Oliveira ‘Savinho’ raia wa Brazil.

Mpaka sasa Haaland  amefunga mabao 10 katika mechi tano za kwanza za Ligi Kuu ni mwanzo bora zaidi tangu Pongo Waring wa Aston Villa alipofanya hivyo mnamo 1930.