Haier yaongeza raha Yanga

DAR ESSALAAM; KAMPUNI ya Haier leo imesaini mkataba mpya wenye thamani ya Sh. bilioni 3.3 kuendelea kuidhamini klabu ya Yanga ya Dar es Salaam kwa kipandi cha miaka mitatu.

“Uhusiano wa Haier na Yanga ulikuwa na baraka kubwa. Ni matumaini yetu kuwa mkataba huu mpya utakuja na mafanikio zaidi.

“Leo ni moja ya siku ya kihistoria kwa Klabu yetu. Leo tunatangaza kuongeza mahusiano na Haier, hii ni taarifa njema sana kwa klabu yetu kwenye uimara wa kiuchumi wa timu yetu.

“Mkataba wa awali ulikuwa mzuri sana. Tulifanya vyema sana kwenye mashindano ya shirikisho ambapo tulifika fainali.

“Msimu wa kwanza na Haier tulifika fainali ya Shirikisho Afrika. Mkataba huu utakuwa wa miaka mitatu mpaka mwaka 2028. Nembo za Haier zitakaa mkono wa kushoto kwenye mashindano ya ligi.

“Mkataba huu utakuwa na thamani ya Sh bilion 3.3,” amesema Rais wa Yanga Hersi Said wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo Dar es Salaam leo.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Haier, Ibrahim Kiongozi amesema kampuni yao inajihusisha na vifaa vya kieletroniki vya nyumbani kutoka China na kwamba uhusiano wa Haier, Yanga na GSM umeleta mapinduzi makubwa

“Nimejivunia kuwa sehemu ya watu ambao wamewezesha mahusiano baina ya Haier, GSM na Young Africans SC. Nawashukuru sana Young Africans kwa mchango wao mkubwa kwenye kutangaza bidhaa za Haier na nembo yetu kiujumla.

“Ni matarajio yetu mahusiano haya yatadumu na kuwa na tija kwa siku zijazo,” amesema Leon Chi Mkurugenzi wa Kanda Haier.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button