HAITI : MAREKANI imelaani vikali mauaji ya watu 200 ambayo yanadaiwa kufanywa na wanachama wa magenge ya uhalifu nchini Haiti.
Msemaji wa ikulu ya Marekani, Karine Jean-Pierre amesema kuwa ripoti hiyo imeishtusha Marekani.
Mwanzoni mwa wiki hii , Ofisi ya waziri mkuu wa Haiti ilidai kuwa watu 180 ambao vikongwe waliuawa katika eneo la Cite Soleil baada ya kushambuliwa. SOMA: Watu 70 wamekufa Haiti
Shirika moja lisilo la kiserikali lilisema kuwa mashambulizi hayo yalifanywa na kiongozi mmoja wa genge la uhalifu ambaye anadaiwa mwanawe kufanyiwa mambo ya kishirikina.