“Hakuna ukiukwaji sheria uandikishaji wapiga kura

MSIMAMIZI wa uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini, Kisena Mabuba amesema hakuna ukiukwaji wowote wa sheria na taratibu katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la mkazi kama ambavyo baadhi ya vyama vya siasa vimelalamika.

Mabuba amesema hayo kwenye Mwalo wa Katonga Manispaa ya  Kigoma Ujiji akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari wakati wa zoezi la uhamasishaji jamii kujitokeza katika zoezi la uandikishaji kwenye daftari la mkazi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mabuba ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji amesema vyama vyote vilitakiwa kuweka mawakala kusimamia taratibu hizo lakini vituo vingi havina mawakala wa vyama na hata waliopo hawakai vituoni muda wote hali inayofanywa kutoa taarifa za uongo kwa viongozi wao wanaporudi na kukuta takwimu za kuongezeka kwa idadi ya wananchi walioandikishwa.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Mwenyekiti wa ACT Wazalendo jimbo la Kigoma Mjini, Halfan Bona alisema kuwa wanao Ushahidi wa kufanyika kwa vitendo vya ukiukwaji wa kuongeza majina ya watu ambao hawakufika kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura akituhumu jambo hilo kuwa na maelekezo ya viongozi wa CCM.

Habari Zifananazo

Back to top button