Hakuna ushuru magari ya gesi, umeme
SERIKALI inakusudia kusamehe ushuru wa bidhaa unaotozwa kwa mujibu wa uwezo wa injini (engine capacity) kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme pekee yanayotambulika kwa HS Code 8702.40.11; 8702.40.19; 8703.80.10 na 8703.80.90 na magari yanayotumia Nishati ya Gesi Asilia (CNG) pekee.
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ameyasema hay oleo katika hotuba yake ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
“Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya nishati ya umeme na gesi asilia nchini na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni inayotumika kuagiza nishati ya mafuta kutoka nje ya nchi.”Amesema