Guterres aonya kuhusu sudan

MAREKANI : KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali inayoendelea kuwa mbaya katika mzozo wa Sudan wakati alipokutana na mkuu wa majeshi wa Sudan, Jenerali Abdel-Fatah Al-Burhan, katika mkutano wa hadhara mjini New York.

Taarifa kutoka Umoja wa Mataifa inabaini kwamba Guterres alionesha wasiwasi mkubwa juu ya machafuko yanayoongezeka nchini Sudan, ambayo yanatarajiwa kuwa na athari kubwa kwa raia. Aidha, kuna hofu kuwa machafuko haya yanaweza kuenea katika ukanda huo.

SOMA Sudan yakataa ujumbe wa umoja wa mataifa

Afisa Mkuu wa Uratibu wa Misaada wa Umoja wa Mataifa, Joyce Msuya, aliongeza kuwa watu nchini Sudan wamevumilia miezi 17 ya hali ngumu na mateso yao yanaendelea kuongezeka.

Habari Zifananazo

Back to top button