Hamas yakubali kusitisha vita Gaza

GAZA, PALESTINA: KUNDI la Hamas limetangaza kukubali pendekezo jipya la kusitisha vita kwa muda mfupi katika Ukanda wa Gaza.
Afisa wa ngazi ya juu wa kundi hilo, Bassem Naim, amesema wamekubaliana na mapendekezo hayo bila kutoa maelezo zaidi. Vyanzo vya upatanishi kutoka Misri na Qatar vimeeleza kuwa makubaliano hayo mapya yanataka Israel kuondoa vikosi vyake ndani ya Gaza na kutoa ahadi ya kuanzisha mazungumzo ya kudumu ya amani.
Kwa upande wake, Hamas imekubali kuwaachia kwa awamu baadhi ya mateka wa Israel wanaokadiriwa kufikia 50. SOMA : Hamas yakataa mpango wa Trump



