Mobeto apokea ubalozi mpya.

DAR-ES-SALAAM: Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameendelea kufanya vizuri katika kazi zake na kupata ubalozi wa bidhaa ya Spaghetti huku akisema juhudi zake katika kazi zimemwezesha kupata nafasi hizo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuwa balozi Hamisa amesema kuwa kupenda kwake kupika na kula imepelekea  kuwa rahisi kwake kupata fursa ya ubalozi huo.

Amesema licha ya kwamba ni mwanamitindo hapendi kujibana kula kama wengine anahitaji kujenga afya yake ili kuwa katika muonekano mzuri unaopelekea kuwa balozi.

Advertisement

“Kila mtu ana vitu anavipenda, napenda kula na ndio maana nafanya kazi kwa bidii na Mungu ananipa fursa kama hizi za ubalozi wa bidhaa za tambi, niwashukuru wote wanaonifikiria kwa kunikaribisha kuwa mwanafamilia niwaahidi sitawaangusha nitafanya kazi vizuri,”amesema Hamisa.

SOMA: Hamisa yuko tayari kuacha muziki

Hadi sasa Hamisa ni miongoni wa wasanii wa kike kwa mwaka huu waliochukua ubalozi kwa kasi tangu mwaka kuanza.