Harmonize aachia rasmi Muziki wa Samia

Rajabu Abdul 'Harmonize'

MTANDAONI:Msanii wa bongo fleva Rajabu Abdul ‘Harmonize’,  ameachia rasmi albamu yake ya tano ijulikanayo kama Muziki wa Samia.

Msanii huyo amechapisha kupitia mitandao yake ya kijamii Juni 3,2024 na kusema albamu hiyo itakuwa na nyimbo 10.

Amezitaja kuwa ni Tanzania, ⁠Samia Tena, Tunatamba Nae,  ⁠Anatekeleza, ⁠Mama Anajenga, ⁠Mama Teacher, ⁠Kazi Iendelee, ⁠Tuvushe, ⁠Na Nusu na ⁠Wanajisumbua.

Advertisement