Hekari 807 za bangi zateketezwa

11 mbaroni

MARA: MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa, Askari mgambo limefanikiwa kuteketeza hekari 807 za mashamba ya bangi.

Pia, limekamata  gunia 507 za bangi kavu iliyo tayari kusafirishwa, gunia 50 za mbegu za bangi pamoja na  kuteketeza viwanda viwili vidogo vilivyokuwa vikitumika kuchakata na kufunga bangi kabla ya kusafirishwa.

Mamlaka hiyo pamoja na vyombo vingine vya dola, imefanikiwa kuteketeza kiasi hicho cha dawa katika operesheni maalum mkoani Mara hususani katika kanda maalum ya Tarime Rorya kwenye bonde la mto Mara iliyofanyika kuanzia Oktoba 2 hadi 8 mkoani humo.

Katika operesheni hiyo pia, watuhumiwa 11 wamekamatwa wakihusishwa  na dawa hizo.

DCIM100MEDIADJI_0676.JPG

Akizungumzia tukio hilo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, wakazi wa eneo hilo wamelifanya bonde la mto Mara kama eneo maalum kwa ajili ya kilimo cha bangi na kujimilikisha.

“Wamejimilikisha, hawaruhusu mtu yeyote asiye mkazi kuingia kwenye bonde kama sehemu ya kuficha uhalifu wao.” Amesema Lyimo na kuongeza

“Wametishia kumdhuru  yoyote atakayeingia ndani ya bonde hilo bila ridhaa yao. Pia, wamediriki kufunga ofisi ya kijiji wakimtuhumu mtendaji wa kijiji cha Nkerege kutounga mkono kilimo cha bangi.

“Uwepo wa daraja lililopo katika moja wapo ya vijito vinavyopeleka maji mto Mara, linatumika kama kizuizi cha watu kwenda kwenye hifadhi ya bonde la mto maeneo yanayolimwa bangi.”Amesema

Amesema, ili mtu avuke anatakiwa kujieleza nia na madhumuni ya kuvuka kuelekea upande wa pili, na wahusika wasiporidhika na maelezo hawakuruhusu kuendelea na safari.

Ameongeza kuwa, baadhi ya viongozi wasio waaminifu wa vijiji vinavyopakana na bonde hilo pamoja na wananchi waliojimilikisha bonde hilo muhimu kwa uchumi wa taifa, wamekuwa wakikodisha na kuuza mashamba ya kulima bangi ndani ya hifadhi ya bonde hilo.

Aidha, kutokana na mto Mara kuwa muhimu sana katika ikolojia ya mbuga ya Serengeti, Kamishna Jenerali Lyimo ameomba Wizara zinazohusika kushirikiana na Mamlaka kutokomeza kilimo cha bangi katika eneo hilo, kwani licha yai operesheni iliyofanyika bado mashamba ya bangi ni mengi pembezoni mwa mto na wananchi wamekuwa wakitumia maji ya mto kumwagilia.

‘‘Tukiacha kilimo cha bangi kiendelee hivi, na kuwaacha wananchi waendelee kuchepusha maji ya mto kumwagilia bangi mwisho wa siku itaharibu ikolojia katika mbuga ya Serengeti na mto kwa ujumla. “Amesema

Amesema, ni vema Mamlaka za serikali zikashirikiana kuhakikisha eneo hilo linasimamiwa vema ili kufanikisha kusitishwa kwa kilimo cha bangi.

Sambamba na hilo, amewataka viongozi wa serikali za mitaa waliotoroka kuwa sehemu ya mapambano ya dawa za kulevya kwa kuhakikisha kwamba, wanakomesha kilimo cha bangi watakaporejea.

Pia, Kamishna Lyimo amesema, Mamlaka kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara na uongozi wa wilaya ya Tarime, watafanya mikutano ya hadhara na kufikiria kuwa na mipango kabambe kuona ni namna gani bonde litalindwa dhidi ya kilimo cha bangi na uhalifu mwingine.

‘‘Sisi kama Mamlaka tutafanya operesheni endelevu katika maeneo haya kuhakikisha kilimo cha bangi kinaisha. Bonde hili lina rutuba nyingi na linakubali mazao ya aina zote, hivyo tumekubaliana na mkuu wa mkoa wa Mara kuwa na mikakati ya kusimamia bonde ili kumaliza kilimo cha bangi na kutafutwa kwa shughuli nyingine ambayo itakuwa rafiki’’ amesema Lyimo.

Nae diwani wa kata ya Tulwa Chacha Machugu amesema, viongozi wa serikali za mitaa wanaosaidia kuendelea kwa kilimo cha bangi wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine

Aidha, amewaomba viongozi wa dini kusaidia kuwaambia waumini wao  kuwa dawa za kulevya hazitakiwi.

‘‘Tutashirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha bangi hailimwi Tarime na yeyote atakaye kiuka miongozo na sheria za nchi atawajibishwa kwani sote tunaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “amesema.

Magreth Ally mkazi wa Tarime amesema kuwa, vijana wengi wanalima bangi kwa madai ya kupata fedha kwa haraka. Hivyo, ameiomba serikali kutoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya, kuelekeza na kuwezesha kilimo cha mazao mbadala ili kuepusha kurithishana kilimo cha bangi kama njia pekee ya kujipatia kipato kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Akizungumzia operesheni iliyofanyika, Isaya Banda mkazi wa Tarime, ameiomba serikali kufanya operesheni endelevu katika maeneo yote ili kutokomeza bangi kwani vijana wengi wameathirika na matumizi ya dawa hizo.

Pia, amewaomba wananchi kuwafichua wanaojihusisha na kilimo na biashara ya bangi.

Kwa upande mwingine Chacha Michael mkazi wa kijiji cha Nkerege ambako operesheni hii imefanyika, ametoa msimamo wake juu ya kilimo cha bangi kwa kusema; “Hili zao linatuharibia sana vijana wetu, wanaacha kusoma wanaenda kuvuta bangi, vilevile tunauomba uongozi wa mama Samia zoezi hili liwe endelevu kwa sababu hapa mto Mara kilimo cha bangi kimekithiri sana. Kuna mazao mengi ya kulima ukapata hela kila zao linakubali hapa Tarime lakini wengi wamekimbilia bangi, mimi sikubaliani nalo kabisa” amebainisha Chacha.

Ekari 101 za bangi zateketezwa

Operesheni iliyofanyika mkoani Mara ni mwendelezo wa  operesheni zilizofanyika katika  maeneo mbalimbali hapa nchini kama moja ya hatua za muhimu katika kupunguza upatikanaji na usambazaji wa dawa za kulevya hapa  Nchini.

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work AT Home
Work AT Home
1 month ago

Earn money in USA, high scores from trusted resources. Work at your own pace. Regular Payments. Search in different job categories. Work anywhere on your vs03 computer, laptop or mobile phone. Update your profile at any time.
.
.
Detail Here———->>> http://Www.Smartcash1.com

Gloria Richardson
Gloria Richardson
Reply to  Work AT Home
1 month ago

I’m making $90 an hour working from home. I never imagined that it was honest to goodness yet my closest companion is earning 16,000 US dollars a month by working on the connection, that was truly astounding for me, she prescribed for me to attempt it simply. Everybody must try this job now by just using this website.. http://Www.Easywork7.com

Last edited 1 month ago by Gloria Richardson
HayleyMelinda
HayleyMelinda
1 month ago

[ JOIN US ] I am making a good salary from home $16580-$47065/ Dollars week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. (i 99q) I thank God every day I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started.…………> http://Www.SmartCareer1.com

Garages&ServiceStations
Garages&ServiceStations
1 month ago

PATA HUDUMA YA MATENGENEZO YA MAGARI KWA MATATIZO YOTE GARI YAKO NA POPOTE ULIPO TANZANIA

NA

MOVABLE KURASINI GARAGE SERVICE STATION

Address: Dar Es Salaam,

,Post Office box: 21493,

Phone number:

022 285 1500

Categories: Garages & Service Stations.

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.jpg

– PIGA SIMU TUKUHUDUMIE

Garages&ServiceStations
Garages&ServiceStations
1 month ago

PATA HUDUMA YA MATENGENEZO YA MAGARI KWA MATATIZO YOTE GARI YAKO NA POPOTE ULIPO TANZANIA

NA

MOVABLE KURASINI GARAGE SERVICE STATION

Address: Dar Es Salaam,

,Post Office box: 21493,

Phone number:

022 285 1500

Categories: Garages & Service Stations..

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.jpg

– PIGA SIMU TUKUHUDUMIE

Back to top button
5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x