‘Hifadhi ya barabara isitumike kutupa uchafu’

DAR ES SALAAM; Wananchi wametakiwa kulinda na kuhifadhi miundombinu kwa kufanya usafi binafsi na kuacha kutupa taka barabarani, kwani makopo na uchafu mwingine huziba mitaro na mifereji ya kusafirishia maji.

Akizungumza leo katika semina iliyoandaliwa kwa Jumuiya ya Waandishi wa Habari wa Mitandaoni (JUMIKITA) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) jijini Dar es Salaam, Dk. Makene Mandoshi, ambaye ni mkuu wa kitengo cha mazingira na jamii TARURA, amesema kila mwananchi ana jukumu la kulinda usafi wa mazingira.

“Askari wa kwanza wa kulinda usafi ni jirani. Tukianza kurekodi video za watu wanaochafua mazingira, itasaidia kufanya jiji letu kuwa safi, kwani kila mtu atakuwa makini akijua anaweza kurekodiwa,” amesema Dk Mandoshi.

Ametoa wito kwa wananchi kushirikiana katika kutunza mazingira bila kusubiri viongozi wa TARURA au TANROADS wawahamasishe.

“Tuanze sisi wenyewe kutunza mazingira yetu. Tunapohifadhi mitaro na mifereji, maji hayatatuama barabarani, hali itakayopunguza foleni na kurahisisha usafiri,” amesema Dk  Mandoshi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button