Hispania vs Italia: Kipute cha kibabe Euro 2024

WAKATI wenyeji Ujerumani imekuwa nchi ya kwanza kufuzu 16 bora katika fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya(EURO 2024), michuano hiyo inaendelea leo huku mchezo kati ya Hispania na Italia ukisubiriwa kwa hamu.

Italia ni bingwa mtetezi wa kombe hilo ambapo mchezo huo wa kundi B utafanyika kwenye uwanja wa Veltins uliopo mji wa Gelsenkirchen.

Katika mechi za kufungua dimba, Hispania iliikanda Croatia mabao 3-0 wakati Italia iliibamiza Albania mabao 2-1.

Hispania na Italia zimekutana mara 41, Hispania ikishinda 13, Italia 11 na zimetoka sare mara 16.

Michezo miwili ya kundi C itabingwa leo, Slovenia ikiikabili Serbia kwenye uwanja wa Allianz jijini Munich wakati Denmark itachuana na England kwenye uwanja wa Deutsche Bank uliopo jiji la Frankfurt.

Habari Zifananazo

Back to top button