IAEA, TAEC kusafirisha mabaki vyanzo vya mionzi

DAR ES SALAAM; SHIRIKA la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), kwa kushirikiana na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), wamekubaliana na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kuanza mchakato wa kusafirisha mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi yake katika mashine za kutibu saratani.
Makubaliano hayo yamefikiwa katika kikao kilichomkutanisha Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk Diwani Msemo, ujumbe wa IAEA kupitia kampuni ya Institute of Isotopes Co. Ltd kutoka Hungary, ukiongozwa na Gábor Kaszás, pamoja na wajumbe kutoka TAEC.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, mabaki ya vyanzo hivyo vya mionzi yatasafirishwa kwenda Hungary kwa ajili ya kuhifadhiwa na kufanyiwa mchakato wa kuyahuisha kwa matumizi mengine, kwa kuzingatia taratibu na viwango vya usalama vinavyotumika katika usimamizi wa vyanzo vya mionzi.
Vyanzo hivyo vimetajwa ni aina ya Cobalt vilitumika katika mashine za tiba ya mionzi kwa vipindi mbalimbali kuanzia mwaka 2008, huku vingine vikitumika kati ya mwaka 2014 na 2020 na mwaka 2025.
Imeelezwa kuwa baada ya nguvu ya vyanzo hivyo kupungua na kutofikia kiwango kinachohitajika kwa ajili ya kutoa matibabu, ORCI ilinunua vyanzo vipya ili kuhakikisha huduma za matibabu ya saratani zinaendelea kutolewa kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama.
Mchakato wa kuondoa na kusafirisha mabaki ya vyanzo vya mionzi ni sehemu ya taratibu za kawaida za usimamizi wa vyanzo hivyo, zinazotekelezwa kwa ushirikiano wa mamlaka husika za ndani, TAEC na IAEA.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi yake yanadhibitiwa na kusimamiwa kwa usalama, huku vyanzo vipya vikiendelea kutumika katika kutoa huduma za tiba ya mionzi kwa wagonjwa wa saratani.
Hatua hiyo pia inaashiria kuendelea kwa ushirikiano kati ya Tanzania na IAEA katika kuimarisha usalama wa matumizi na usimamizi wa teknolojia ya nyuklia katika sekta ya afya.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…………
.
More Details For Us→→→→ https://Www.Payathome9.Com