Idadi ya majeruhi Hanang yapungua

MANYARA: Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dk. Festo Dugange amesema idadi ya majeruhi wa mafuriko ya tope Hanang mkoani Manyara wanaoendelea na matibabu imepungua kutoka 117 hadi 36 na Sh.

buy nizoral online http://medexhco.com/pics/outlook/jpg/nizoral.html no prescription pharmacy

milioni 560 zimetolewa kwaajili ya huduma za afya kwa wathirika hao.

Dk. Dugange  ameambatana Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera,Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama na mhandisi, Godfrey Kasekenya Naibu Waziri wa Ujenzi katika ukaguzi wa maeneo yaliyoathirika ambayo serikali inayarejesha kwenye hali yake katika Mji wa Katesh Wilaya ya Hanang.

buy ventolin online http://medexhco.com/pics/outlook/jpg/ventolin.html no prescription pharmacy

“Tunauhakika hao 36 waliobaki wataendelea kuruhusiwa kurejea nyumbani kuendelea na majukumu yao na jambo la muhimu kwenye majanga haya serikali inajitahidi kudhibiti magonjwa ya mlipuko kujitokeza na sehemu kama hii tulichokifanya tumeimarisha mfumo ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye jamii yetu na katika kambi zetu”amesema  Dk. Dugange

Aidha,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu ,Jenista Mhagama amesema serikali imeanza mazungumzo na taasisi za kifedha ili kutoa unafuu kwa wafanyabiashara walioathiriwa na mafuriko na ameendelea kushukuru wadau wanaoendelea kutoa msaada.

Pia,Waziri Jenista Mhagama amesema mbali na Serikali kurejesha miundombinu pia imeendelea kuwa bega kwa bega na wananchi sambamba na kutoa maagizo kwa Wataalamu wa Satellite kuanza kuangalia Kaya zote na kuona zipi zimeathirika zaidi huku ikiendelea kutoa msaada zaidi.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya amesema hadi sasa urejeshaji wa miundombinu ya barabara na makalvati yaliyoharibiwa na maporomoko ya tope na mawe yaliyotokea Desemba 3, 2023 kwenye Mji wa Katesh wilayani Hanang mkoani Manyara umefikia asilimia 75.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button