IDRAS kuwezesha upatikanaji TIN namba

SHINYANGA: MFUMO Jumuishi wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) unawezesha kuingia na kupata TIN Namba bila kwenda kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuipata kama ilivyokuwa awali mpaka uende ofisini.

Pia ukitaka kubadilisha namba ya simu ilikuwa changamoto ya kukutaka ufike ofisini nakuandika barua ueleze upotevu huo.

Hayo yamesemwa leo na ofisa msimamizi wa kodi kutoka mkoa wa kikodi Kahama, Jaliwa Wilson alipokuwa akitoa elimu kwa wafanyabiashara ,wasimamizi wa wamiliki wa Kampuni juu ya mfumo mpya wa IDRAS ambao umekuja na maboresho zaidi.

Wison amesema mfumo utawezesha kujisajili mwenyewe moja kwa moja kwa kupata huduma 15.

Wilson amesema Ukipoteza simu nakutaka kubadili namba ya simu uliyokuwa umeiandika TRA kuna maswali kumi na moja utaulizwa ukiingia kwenye mfumo lengo kujua uhalali wako wa namba hiyo.

Wilson amesema baadhi ya Watu walikuwa wakifanya udanganyifu kupitia simu za mkononi nakuunganisha TIN namba husika na maafisa TRA kutojua huo kama ni udanganyifu inakuwa ni ngumu mtu akija kulalamika.

“Kufutiwa madeni ulikuwa ni mchakato mkubwa mtu lazima alikuwa aandike barua aje ofisni inakuwa ni usumbufu lakini kupitia mfumo huu mpya utarahisisha hata kama unapingamizi la deni kulikataa utaingia kwenye mfumo na kueleza na badaye kupata majibu” amesema Wilson.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button